Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauaji ya AKA: Washukiwa sita wakamatwa

Mauaji Ya AKA: Washukiwa Sita Wakamatwa Mauaji ya AKA: Washukiwa sita wakamatwa

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Washukiwa sita wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya rapa maarufu wa Afrika Kusini, Kiernan Forbes, maarufu kwa jina la AKA, na rafiki yake wa karibu, mpishi maarufu na mjasiriamali Tebello "Tibz" Motshoane.

Wawili hao waliuawa kwa kupigwa risasi nje ya mkahawa mmoja mjini Durban mwaka mmoja uliopita, katika mauaji ambayo yaliwashangaza Waafrika Kusini.

Polisi walisema wahusika walilipwa ili kumlenga AKA lakini hakuna nia iliyofichuliwa.

Katika taaluma yake, alikuwa na nyimbo nyingi zikiwemo alizomshirikisha Burna Boy wa Nigeria.

Washukiwa hao, wote wenye umri wa chini ya miaka 36, ​​wanatazamiwa kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi.

"Ilikuwa wazi kwamba AKA alifuatiliwa kutoka uwanja wa ndege na Tibz hakuwa mlengwa aliyekusudiwa katika mauaji kwenye Barabara ya Florida huko Durban," Luteni Jenerali Nhlanhla Mkhwanazi, kamishna wa polisi wa jimbo la KwaZulu-Natal, alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne usiku.

"Tunajua walilipwa kwa hili," Luteni Jenerali Mkwananzi aliongeza.

Chanzo: Bbc