Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maua Sama ampiga dongo Zuchu

MAUA SAMA DONGO ZUCHU Maua Sama ampiga dongo Zuchu

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Japo hajamtaja jina lakini kwa asilimia kubwa inaonesha wazi, msanii wa Bongo Fleva Maua Sama ametupia kijembe mrembo kutoka WCB, Zuhura Othman 'Zuchu'.

Hiyo inajidhihirisha kufuatia kauli yake aliyoiposti kenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika hivi:

"Maisha haya! Maroboti yameanza kuoneana Wivu."

Mwishoni alimalizia kwa kuweka viemoji vya kucheka. Kwa nini inaonesha amemlenga Zuchu? Jana kwenye ukurasa wake wa Instagram kipengele cha Insta Story, Zuchu aliweka stori kuwa anawashangaa wasanii wanaonunua views.

Bila shaka alimlenga Zuchu maana ndiye aliyeonesha kuwashangaa wasanii wanaonunua views kupitia maroboti ya YouTube.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live