Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maua Sama amfungulia kesi ya madai Mwijaku, ataka alipwe Mil. 300

Maua Sama Amfungulia Kesi Ya Madai Mwijaku, Ataka Alipwe Mil. 300 Maua Sama amfungulia kesi ya madai Mwijaku, ataka alipwe Mil. 300

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa zimepita siku chache tangu muigizaji na mtangazaji Mwijaku kumzungumzia mwanamuziki Maua Sama sasa #Maua kupitia wakili wake Claudio Msando, wamemuandikia Mwijaku hati ya madai huku ikimpa saa 24 ya kujibu tuhuma hizo za udhalilishaji pamoja na fidia ya tsh 300 milioni.

Kufuatiwa na hati hiyo pia imeeleza kuwa endapo #Mwijaku atashindwa kufanya hivyo basi kesi hiyo itapelekwa mahakamani kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Ukiachiliambali kuchapishwa kwa hati hiyo, hata hivyo Mwijaku kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya jana alimuomba msamaha mwanamuziki huyo kwa maneno aliyoyazungumza kama yamemuumiza kwa namna yoyote ile kwani yeye alichukulia utani kutokana na wawili hao kuzoea kutaniana.

Ikumbukwe kuwa Mwijaku alizungumza maneno hayo yaliyotafsiriwa kuwa ya udhalilishaji wakati alipokuwa kwenye usiku wa miaka 20 ya #King.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live