Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maua Chenkula adai 'kifo' kilimpoteza

Batch Maua Chenkula Maua Chenkula

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa nyimbo za Asili Maua Chenkula amesema kitendo cha kuzushiwa kuwa amefariki kimemuathiri kwa kiasi kikubwa katika tasnia yake ya muziki.

Maua amebainisha kuwa ilifikia kipindi akawa hapigiwi simu hata na marafiki wake wa karibu kwani wengi walijua kuwa amefariki, amedai kuwa ilikuwa vigumu kwa yeye kupata kazi au mialiko mbalimbali ya kufanya matamasha kwani ilifahamika amefariki.

Maua amedai kuwa mwanzo alichukuliwa jambo hilo kawaida, lakini kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo alivyoona athari hasi katika muziki wake.

“Walivyosema umekufa ukawa huonekani tena kwenye macho ya watu, lakini mimi ulitangazwa msiba nikawepo kwenye macho ya watu! Lakini bado ukienda sehemu nyingine tofauti mtu mwingine akikuona anauliza mbona umefanana na Maua ni ndugu yako? Nilikuwa Napata wakati mgumu sana kuwaelewesha kama ni mimi sijafa.” Alisema Maua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live