Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matonya ni icon wa Bongo Fleva

Dsf Matonya S Matonya ni icon wa Bongo Fleva

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: Luqman Maloto

Imewahi sana au imechelewa? Pengine haukuwa muda sahihi. Ukweli ni kuwa Bongo Flava Honors ya Matonya, imeleta confusing opinions.

Kama ilipaswa kufanyika kabla, pengine ilitakiwa ichelewe, au kama vipi irudiwe. Matonya did a wonderful job kiotani Alliance Francaise.

Can you imagine, sauti iliyoimba Uaminifu mwaka 2003, ndiyo hiyohiyo aliyo-perform Bongo Flava Honors 2024? Vocals za Siamini na Vaileti, zilikuwa zilezile. Hakuna changes. Halafu halisi zaidi kwa live band.

Matonya, mwite young maestro. Alivyo-perform track kwa track bila papara na kwa chemistry ya hali ya juu with Swahili Blues Band, unabaki na swali kichwani; Matonya angefanya kazi ipi nyingine zaidi ya muziki?

Ona alivyoanza! Dunia Mapito. Dancers wake wamevaa dera nyeusi. Taifa limetoka kwenye maombolezo ya kifo cha Mzee Rukhsa. Kabla yake, alifariki dunia Edward Lowassa. Tonya ana-connect show ya Dunia Mapito na misiba mfululizo.

Siamini inafuata. My God! Kila mtu ukumbini anaimba. Inafuata Uaminifu. Mpaka hapo ikathibitika bila chembe ya shaka kuwa Matonya ni bankable megastar, halafu ni kipenzi mno cha warembo.

Tonya ana hits nyingi. Wimbo kwa wimbo, aliifanya audience iimbe naye utadhani choirmaster with his own choir. Kuanzia mkwaju wa kwanza mpaka wa mwisho, Tonya delivered a high-energy performance.

Halafu, kulikuwa na surprise appearance ya Fid Q. Good heavens! Unalijua balaa la Fareed wa Mwanza, anaposhika microphone. Hadhira ilikuwa overhyped ikihudumiwa live ngoma ya “Taxi Bubu” na tonic ya “Usinikubali Haraka.”

Kila wimbo ilikuwa kama movie na main character ni Matonya. Spare Tairi hadi Anita, Unanimaliza mpaka Zilipendwa. Zaidi ya dakika 150, Tonya na jukwaa, bado ana nguvu ya kuendelea kushusha vyuma na audience haikutaka ashuke jukwaani.

Jambo ambalo angalau lilikuwa mwafaka wa pamoja kwa kila aliyehudhuria Bongo Flava Honors ya Matonya ni kuwa Matonya’s performance is iconic, na imempambanua kuwa miongoni mwa wanamuziki bora wa Bongo Flava wa muda wote.

Sugu’s Moto Chini performance was epic. Frontyard to backyard, watu walising along “Moto Chini”. DJ Boniluv sasa, aisee yule mkongwe alizaliwa kucheza na sahani.

Chanzo: Luqman Maloto