Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matonya alivunja Katiba ya Bongo Fleva, hakushtakiwa

Matonyambili 57336623 135595310902135 3798834724364761925 N Msanii Matonya

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpango kazi wa Tanga kuitawala Bongo Flava, ulitambulisha silaha yao Matonya, ambaye kinyonge, alilia “Uaminifu” akimshirikisha Bwana Misosi.

Jamhuri yote ya Bongo Flava ilisaluti talanta ya Matonya. Halafu akapotea. Tanga ikachekwa kuwa ilitambulisha silaha “one hit wonder”. Ngoma moja, pumzi kwisha.

Hesabu 2004, nenda 2005, weka kituo 2006. Matonya akarudi kwa ujio ulioacha historia dude baada ya dude.

“Siamini” ilikuwa chereko. Janki wa Kitanga aliopoa manzi mwenye mahaba ya kibaikoko na kidumbaki, hakuamini. Halafu huyo manzi, kawatosa matajiri wenye mzigo.

Ujio wa pili, Matonya hakutaka mazoea. Siamini haijapoa, akaifanya Afrika Mashariki ilie kwa “Dunia Mapito.” Zikafuata tambo za kumpata “Vailet”. Sijui nani alichonga Tonya asingempata Vai wake!

Ngoja nikusimulie mshikaji wangu, Vailet ni mkwaju uliokaa kileleni kitambo kirefu bila kushuka wala kuchoka. Taifa likashudia ma-Vailet wengi. Walijitokeza kwenye vyombo vya habari, wakisema ni wao walioimbwa. Ni Bongo Flava na drama zake.

Wanamuziki wanadumu na mapenzi basi? Ilipofika mwaka 2008, Matonya alikwenda mpaka kwa mganga kumsaka “Anita”. Kazi ya Ambrose Dunga. Mom In Chief wa Bongo Flava, Lady Jaydee, aliweka sauti.

Ni Matonya aliyemfanya Irene Uwoya aitwe “Taxi Bubu” kwa kolabo na Fid Q, halafu akampigia magoti Aunty Ezekiel, ili tu amkubalie kuwa “Spare Tyre” mbele ya njemba yake, Mpoki.

Katiba ya Bongo Flava inatambua muhula wa utawala kimuziki ni mwaka mmoja bila nyongeza. Mwaka 2006, Matonya alipokaa on top, alivunja Katiba, akabaki madarakani 2007, 2008 hadi 2009. Raia walichekelea Tonya kuvunja Katiba.

Wengi hamjui how good the good old days, Matonya akiitawala Bongo Flava kama mali yake binafsi. Mapromota waliteseka kumpata. Bookings zimefunga mwaka mzima. Hakuna upenyo. Kila siku ziarani.

Nini nyumba na magari? Matonya alijenga mpaka hoteli. Unashangaa? Kwani ule u-busy, mwaka mzima anapiga show bila kupumzika, alikuwa anaingiza mawe?

Ukifika Alliance Francaise, Upanga, Februari 23, 2024, utakuwa mwenye bahati sana kuujua ukuu wa Matonya. Sugu The Jongwe, DJ Boniluv na Swahili Blues Band, watakuhudumia.

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live