Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matonya; The Black Card Artist!

Matonyambili 57336623 135595310902135 3798834724364761925 N Matonya; The Black Card Artist!

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: Luqman Maloto

Sera ya “divide and rule” ya Wakoloni, ilileta utengano wa maskani za kuishi; Uzunguni, Uhindini na Uswahilini. Watoto wa Uswahilini wakawa daraja la mwisho kimaisha.

Uswahilini mitaa bila mipangilio, huduma za kijamii tabu tupu, kipato nacho mtihani. Watoto wa Uswahilini waliwaonea gere wa Uzunguni na Uhindini. Matamanio yao yakawa kuishi Uhindini au Uzunguni, lakini ilioneka ni impossible to upgrade the level.

That lad, Matonya, story yake ni “impossible getting done”. Balaa kubwa alilolitengeneza kupitia mauzo ya albamu “Siamini”, aligeuza ndoto kuwa kweli. Alivamia Uhindini, akanunua mjengo mkali. Akamwambia bi mkubwa wake: “Mama, kuanzia sasa wewe ni mkazi wa Uhindini. Siyo tena Uswahilini.”

Hii siyo hadithi ya Bongo Flava ilivyobadili maisha ya vijana from grass-to-grace, bali jinsi muziki huo ulivyowafanya vijana wenye vipaji kutoka Uswahilini, watunishe wallet kwenye maskani za wenye upendeleo na kuishi nao mtaa mmoja.

Hakuna uchawi unaoweza kukiroga kipaji chenye radhi ya kifedha kutoka kwa Muumba. Hits back-to-back alizoachia, zikamfanya Matonya amiliki “Black Card”, iliyomfungulia milango yote ya VIP.

Enzi zile anaimba “Natafuta Mrembo”, baada ya sonona la “Uaminifu”, alipotoa “Vaileti”, ni yeye ndiye akawa anasakwa na warembo. Mwisho, akaingizwa mkenge na yule “Taxi Bubu”.

Matonya aligeuka topic ya wazee kwenye vijiwe vya bao na kahawa, sababu ya “Dunia Mapito”. Halafu “Anita” ulikuwa content ya vikao vya harakati za wanawake, waliokataa kupelekeshwa na wanaume kama magari mabovu.

Potezea kidogo habari za Matonya kujenga hoteli Tanga, ule u-VIP wake wa Black Card, ulifungua milango ya Serikali, Nairobi, Kenya, akagonga lease. That’s right, Matonya anamiliki ardhi Nairobi. Fedha zilitoka kwenye mgodi wa Bongo Flava.

Machi 8, 2024, Alliance Francaise, Upanga, haitakuwa siku ya Bongo Flava Honors kumpa heshima Matonya, bali kutambua mchango wa askari muhimu kwenye jeshi la Bongo Flava, aliyesimama imara war-to-war, hadi ushindi wa utamaduni ukapatikana.

Baraka iliyoje kuipata huduma ya Matonya live with Swahili Blues Band, kwa zaidi ya dakika 120? Sugu The Jongwe will host the affair.

Chanzo: Luqman Maloto