Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mateso aliyopitia Mzee Korongo dakika za mwisho, mdogo wake asimulia!

Korongo Pic Data Mzee Korongo

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Muigizaji wa filamu Hamis Korogo ’Mzee Korongo, amefariki dunia huku mdogo wake akieleza dakika za mwisho alivyopigania uhai wake.

Mzee Korongo ambaye hivi karibuni alikuwa akionekana kwenye tamthilia ya ‘Kuti Kavu’ alifikwa na umauti jana Jumatatu, Agosti 22, 2022 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Msiba wake upo Mbezi kwa Yusufu na anatarajiwa kuzikwa kesho Jumatano kijijini kwao Dakawa, mkoani Morogoro ambapo leo Jumanne kutafanyika dua nyumbani kwake.

Akisimulia namna ndugu yake alivyopigania uhai wake dakika za mwisho, mdogo wa marehemu, Ramadhan Korongo, amesema ndugu yao alifanyiwa operesheni tatu wiki moja iliyopita.

Hii ni baada ya Agosti 10, 2022 kuumwa tumbo ghafla akiwa nyumbani kwake, hali iliyofanya kupelekea kituo cha afya alichokitaja kwa jina la Kipasuka na alikuwa akitapika damu hali iliyomfanya aongezewe maji na alipopata nafuu aliruhusiwa kurudi nyumbani.

“Usiku wa saa nne hali yake ilibadilika tena, akapelekwa hospitali inaitwa Makondeni, akatundikiwa drip mpaka saa 11 asubuhi na kurudi nyumbani ambapo hakukaa sana hali ikabadilika kwa kupata kwikwi kwa muda mrefu na kulazimika kupelekwa hospitali ya Mbezi.”

Advertisement “Mbezi pale akaongezewa maji chupa nne na baadaye madaktari wakaona hali inazidi kuwa mbaya wakamwandikia rufaa ya kwenda hospitali ya Mwananyama,” amesema Ramadhani.

Mdogo wake huyo ameendelea kusimulia, baada ya kufanyiwa uchunguzi akiwa Mwananyamala, iligundulika kuwa utumbo wake mkubwa umejikunja lakini pia anasumbuliwa na tezi dume ya upande wa kulia na kushoto.

“Basi akashauriwa arudi nyumbani hadi Agosti 12, 20-22 arudi tena hospitali hapo kwa ajili ya upasuaji ambapo alifanyiwa siku ya Jumanne,” amesema.

Ramadhani amesema operesheni hizo zote zilifanyika salama na ilipofika Jumamosi ya Agosti 20, 20222 aliruhusiwa kurudi nyumbani na akawa akizungumza na watu na kuwapa taarifa kuwa anaendelea vizuri.

Amesema, ilifipofika juzi (yaani Jumapili), akawa anatokwa jasho, lakini akishikwa mwili ulikuwa baridi ikabidi arudishwe tena hospitali ya Mwananyamala ambako alifanyiwa upasuaji na wakati huo ilikuwa ni saa tatu usiku.

“Madakatari walimuhoji na baadaye kumpima ambapo iligundulika presha yake imeshuka ambapo majira ya saa saba usiku alirudishwa wodi namba tano ambayo alikuwa akalazwa awali na kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua na baadaye kuongezewa maji.

“Ilipofika saa 11 alfajiri, fahamu zikaanza kumrejea lakini sasa akawa hawezi kuzungumza kwa maneno isipokuwa kwa vitendo na akawa anaonyesha eneo la tumbo kuja juu kuwa ndilo linalomuuma na kueleza alipofanyiwa upasuaji hakuna shida.

“Jambo hili lilitupa matumaini lakini jana Jumatatu saa kumi jioni muda wa kuingia kuwaona wagonjwa, tulipofika tulikuta akiwa amezungukwa na madaktari, alitaka chai tukampa, lakini baada ya hapo mapigo yakaanza kwenda mbio takaambiwa tumuache aendelee na drip na haikupita muda ndipo mwili ukaacha roho (akafariki),” amesema Ramadhani.

Mzee Korongo amefariki akiwa ameacha watoto watano kati yao wa kiume watatu na kike wawili.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz