Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Matangazo ya 'sajari' za maumbo marufuku

Plastic Surgery.jpeg Matangazo ya 'sajari' za maumbo marufuku

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uingereza imeyapiga marufuku matangazo ya kliniki tatu za Uturuki yanayohamasisha upasuliwaji wa mwili kwa ajili ya urembo.

Matangazo hayo yaliyokuwa yakionekana katika mtandao wa Facebook yametajwa kutofaa kwa kutumia lugha yenye ushawishi kuwalenga watu ambao hawana taarifa za kutosha kuhusu madhara ya mambo yanayotangazwa.

Wataalamu wameeleza kuwa watoaji wa huduma hizo hawaweki wazi matatizo yanayoweza kumtokea mtu anayefanyiwa upasuaji huo.

Hadi sasa kumekuwepo na malalamiko mbalimbali ya kiafya pamoja na vifo kadhaa vya wanawake waliofanyiwa upasuaji wa urembo nchini Uturuki.

Mapema mwezi huu mchunguzi mmoja wa maiti nchini Uingereza alisema anayo nia ya kuiandikia barua serikali kwani ana wasiwasi mkubwa juu ya wanawake kutokuyajua matatizo yatokanayo na upasuaji wa urembo.

"Najua huko tunakoelekea watakufa watu wengi ,afadhali tuseme mapema huenda tukaokoa maisha ya mtu hata mmoja".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live