Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Master Jay ‘aogopa’ kuoa akikumbuka yaliyompata Stamina

95953 Pic+stamina Master Jay ‘aogopa’ kuoa akikumbuka yaliyompata Stamina

Mon, 17 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Joachim Kimaro maarufu Master Jay amesema ana jambo la kujifunza baada ya ndoa ya msanii wa Bongofleva, Stamina kuvunjika.

Ametoa kauli hiyo baada ya mtayarishaji huyo kushauriwa na mmoja wa mashabiki zake amuoe mpenzi wake, Sarah Kaisi.

Sarah maarufu  Shah ni  msanii wa Bongofleva aliyewahi kutesa na wimbo wa ‘Sugua Gaga’, amekuwa katika mahusiano na Master Jay kwa muda mrefu.

Jana Ijumaa Februari 14, 2020 katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Master Jay alimtakia Shah heri ya siku ya wapendanao  kwa kuweka picha akiwa amemkumbatia na kuandika, “leo ndio wengi watajua kama wao ni main chick au... Hi! my Valentine Shaa.”

Mmoja wa walioweka maoni katika picha hiyo amesema, “muoane jamani.”

Katika majibu yake Master Jay amesema, “anza wewe ili uishie kama Stamina, hii si uwekezaji mdogo  hivyo hakuna haja ya kuharakisha kwa sababu ya kusukumwa na makundi ya kijamii.”

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz