Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Master J atoa shukrani kupata Shavu BASATA

Master Jay Master J

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Producer maarufu nchini Master J ameteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria ya Baraza Na.23 ya mwaka 1984 sura 204.

Baada ya uteuzi huo Master J kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa shukrani zake kwa waziri Ndumbaro, kwa kumteua kuwa mjumbe, na kuahidi kutimiza wajibu wake kwa uadilifu na weledi kwa ushirikiano na wajumbe wenzake.

Huku ‘mastaa’ wengine walioteuliwa katika baraza hilo ni Single Mohamed Mtambalike (Richie Richie), Jessica Julius Mshama, Dkt. Gervas Andrew Kasiga (Chuma), Felista Steven Lelo na Mgunga Attilio Mwamnyenyerwa. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live