Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa wateswa na msongo wa mawazo

Harmonize 1 Mastaa wateswa na msongo wa mawazo

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KWA nini baadhi ya mastaa Bongo wamekuwa wakilalamika kuteswa na msongo wa mawazo ilihali wanajisifu kuwa na maisha mazuri?

Baadhi ya mashabiki wao wanasema kuwa, licha ya mastaa hao kuwa na pesa na ustaa, lakini mbona baadhi yao wanalalamika kuangamia kutokana na msongo wa mawazo?

Baadhi ya mastaa ambao wamejitokeza hadharani na kudai kusumbuliwa na msongo wa mawazo ni pamoja na Harmonize au Konde Boy kutokana na Kajala kushindwa kumjibu ombi lake la kutaka warudiane.

Wengine ni Vanessa Mdee ambaye ameaamua kuachana kabisa na muziki, Linah Sanga, Ruby, Navykenzo (Aika na Nahreel) na wengine wengi ambao wamewahi kukiri waziwazi kuwa muziki unasababisha msongo wa mawazo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Mtaalam wa Saikolojia na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Chris Mauki, maisha ya mastaa wengi ni magumu kwani hulazimika kubeba shinikizo zaidi kuliko watu wa kawaida.

“Hawawezi kurudi kwenye maisha ya kawaida kwani wanazoea kupewa umakini mwingi kwa kufuatiliwa hivyo kuigiza kuishi maisha ya kifahari wakati katika uhalisia haiku hivyo.

“Inapotokea mtiririko wa pesa au mikataba ikiisha, watu husahau pesa zao na muhimu zaidi ustaa wao umetoweka hivyo wana uwezekano mkubwa wa kushambukliwa na msongo wa mawazo,” anasema mtaalam huyo wa saikolojia na kuongeza;

“Kule kuwa staa kunamaanisha kila wakati unafuatiliwa kwa njia tofauti hivyo lazima waigize kuishi maisha yasiyo ya kawaida na mtu wa kawaida ambaye siyo staa.

“Ni maoni yangu binafsi, lakini ukweli ni kwamba mastaa wengi hawaishi maisha sawa na mtu wa kawaida, jambo linalowafanya kujaribu kuishi maisha yasiyo ya kwao na pale inaposhindikana ndipo unasikia vilio vya kujitumbukiza kwenye uraibu wa pombe, madawa ya kulevya na uhalifu mwingine wa kutaka kujipatia kipato ili kuendana na matakwa ya maisha ya kifahari.

“Pia mastaa wengi wanajikuta kwenye migogoro mingi ya kimahusiano kwani hawana mahusiano thabiti katika maisha ambayo ni muhimu sana kwao.

“Kwa kushindwa au kukosa mambo hayo, hujikuta wakipita kwenye huzuni ambayo hujilazimisha kucheka mbele za mashabiki, lakini wanaungua ndani kwa ndani.

“Mastaa wana shinikizo kubwa na mifadhaiko ambayo m huwaweka kwenye hatari ya kukabiliwa na magonjwa ya afya ya akili na wakati mwingine husababisha shida na hata kuchukua uhai wao; ipo mifano mingi ya hapa Tanzania na ulimwenguni kwa jumla.”

Mtaalam huyo anawashauri kujitahidi kuishi kwenye maisha halisia na kama kuna ambaye ameanza kuona dalili za msongo wa mawazo, basi aanze kutafuta msaada wa haraka kwa wataalam na washauri wa masuala ya kisaikolojia.

Hata hivyo, anasema suala la msongo wa mawazo kwa sasa si tatizo la mastaa pekee, bali ni janga la kitaifa na ulimwengu hivyo linatankiwa mtu binafsi ajue jinsi ya kujilinda kwani linasababisha vifo vya watu wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live