Akili ni nywele, kila mtu ana zake. Baadhi ya wanawake maarufu waliamua kutupilia mbali nywele ndefu wakiwa kwenye umaarufu wao na wengine wao kwenye muziki.
Wanawake hawa waliamua kuwa na nywele fupi kwa sababu zao ambazo wengi wao hawajafichua ila wengine wao imeonekana kuwa ni asili yao ya urembo.
Miongoni mwa hawa wana wake ni:
Nadia Mukami
Mwanamuziki huyo alikuwa na nywele ndefu kwa muda na alikuwa akionekana hadharani na nywele ndefu. Baada ya Nadia kupata ujauzito wake na kujifungua ndipo alipoamua kuzinyoa nywele zake na kutulia na nywele fupi mpaka sasa ila mara nyingine yeye hutumia wigi ama nywele bandia anapoenda kwenye shoo zake.
Femi One
Hitmaker huyu wa 'Utawezana' pia amekuwa akiweka nywele fupi kutoka hapo awali hata alipoanza muziki wake. Ingawa yeye hutumia wigi mara chache zaidi ,mwanamuziki huyu hupaka rangi za aina tofauti kwa nywele yake fupi.
Nana Owiti
Mkewe Kennedy Ombima almaarufu King Kaka pia amekuwa na nywele fupi kwa muda sasa ila pia yeye ako kwenye hiyo ligi ya kuiweka nyele yake rangi. Owiti ni mtangazaji wa kipindi cha Chatspot katika runinga ya Switch.
Wahu
Mwanamuziki Wahu Kagwi ameziweka nywele yake ikiwa fupi kwa muda mrefu sasa. Yeye huziweka nyele yake rangi za aina tofauti kwa wakati mwengine ila hatumii nywele bandia.
Pritty Vishy
Aliyekuwa mpenzi wake Simple Boy huwa ameeka nywele fupi ambayo huwa anaipamba kwa kuiweka rangi ama wakati mwingine yeye huvaa nywele bandia ili kuwafurahisha mashabiki wake.
Vishy juzi baada ya kutangaza kuachana na msanii Madini Classic, anasherehekea kufikisha umri wa miaka 21 Jumatatu hii.
Rue Baby
Mtoto wake mwanamuziki Akothee ambaye pia ni mwanamitindo, Rue baby huwa ameiweka nywele yake fupi kutoka kitambo. Mwanamitindo huyu huwa haiweki nywele yake rangi yoyote ila huwa anaiwacha ilivyo na rangi yale ya asili.
Huddah Monroe
Socialaiti,Huddah ameweka nywele fupi ila yeye hutumia nywele badia wakati mwengine.
Nyce Wanjeri
Mwigizaji huyu pia ni miongoni mwa wanawake maarufu wanaoweka nywele fupi.