Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa wa Nigeria waangukia pua tuzo za Grammy

Mastaa Wa Nigeria Waangukia Pua Tuzo Za Grammy Mastaa wa Nigeria waangukia pua tuzo za Grammy

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: Mwananchi

Kama kuna kitu wasanii wa Nigeria walikuwa na uhakika nacho katika tuzo za 66 za Grammy 2024, ni kuondoka na ushindi mnono kutokana na kuchaguliwa kuwania vipengele vingi, pamoja na kupewa nafasi ya kutumbuiza lakini wamejikuta wakipigwa na kitu kizito.

Tuzo hizo zilizoanzishwa Mei 4, 1959 zikifahamika kama Gramophone, zimetolewa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Crypto.com Arena Jijini Los Angeles nchini Marekani ambapo wasanii wengi wakubwa wa Nigeria walihudhuria.

Burna Boy, mshindi wa Grammy 2021 ndiye msanii wa Nigeria na Afrika aliyechaguliwa kuwania vipengele vinne, Davido vitatu, huku Asake na Ayra Starr wakipata kimoja kimoja.

Naye Davido ambaye ni mara yake ya kwanza kuwania Grammy alitajwa vipengele vya Best Global Music Album (Timeless), Best Global Music Performance (Feel, Unavailable) na Best African Music Performance.

Hata hivyo, Burna Boy, Davido na wenzao wameambulia patupu katika vipengele vyote na sasa watarejea nyumbani kwao bila kitu chochote ambacho hata mashabiki na wadau wao hawakukitarajia hapo awali.

Staa wa Amapiano kutokea Afrika Kusini, Tyla, 22, ndiye msanii pekee wa Afrika aliyeibuka mshindi Grammy 2024 ambapo ameshinda kipengele cha 'Best African Music Performance' baada ya kuwabwaga Asake, Burna Boy, Davido na Ayra Starr.

Ushindi huo unakuja wiki mbili baada ya Tyla anayetamba na wimbo wa 'Water' kusema anaamini atashinda tuzo hiyo kwa kile alichoeleza kama ameweza kuchaguliwa kuwania, basi ushindi pia unawezekana.

Chanzo: Mwananchi