Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Bongo waisusia Kanumba Day

Kanumba.jpeg Steven Kanumba

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama inavyotambulika kila ifikapo April 7, kila mwaka huwa ni siku ya Kanumba day, ni siku ya kumbukumbu ya mfanano na ile siku ambayo umauti ulimchukua Nguli wa sanaa ya maigizo nchini, Steven Charles Kanumba, siku hii huwa ni maalumu kwa kuuenzi na kuupa thamani mchango wa Kanumba katika kuiinua sanaa kiasi cha kujulikana kimataifa.

Katika siku hii, Ndugu, jamaa, marafiki na Mastaa mbalimbali huwa wanafika nyumbani kwa mama Kanumba ili kumfariji na kumuombea Dua mpendwa wao, hata hivyo mwaka huu hali hiyo haijakuwepo ambapo Mastaa wengi wamepuuza tukio hilo, licha ya kuto kwenda kumfariji mama Kanumba lakini hata kwenye kurasa zao za Instagram hawajaandika chochote, hali ambayo inaonyesha hawaoni umuhimu wa tukio hilo kuendelea ingawa hii inaleta picha mbaya kwa mashabiki.

Hata hivyo siyo mwaka huu tu, ni kwa miaka kadhaa sasa wasanii hao ambao wengi wao waliibuliwa na Kanumba wamekuwa wakipuuzia na kususia siku hiyo bila hata kwenda kumjulia hali mama Kanumba.

Licha ya wao kuto kuwepo, lakini hawakuzuia shughuli hiyo kufanyika, ambapo kwa uwezo wake mama Kanumba siku ya jana amefanya hafla fupi pamoja na ndugu jamaa na marafiki wakiongozwa na Zuwena ambao walishiriki ibada na kufanya usafi katika kaburi la mpendwa wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live