Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masogange kuagwa leo

Sun, 22 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

MWILI wa mrembo anayepamba video za wanamuziki wa Bongo Flava nchini, Agness Gerald ‘Masogange’ unatarajiwa kuagwa leo kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni.

Kwa mujibu wa mmoja wa wajumbe wa kamati ya mazishi upande wa wasanii, Steven Mengele 'Nyerere' alisema jana kuwa baada ya kutoa heshima za mwisho mwili huo utasafirishwa kwao Mbeya tayari kwa kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele. Masogange alifikwa na umauti juzi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

"Saa 10 jioni leo (jana), tutakutana Leaders kwa taratibu za mwisho na kukusanya fedha kwa ajili ya kuuifadhi mwili wa mwenzetu," alisema Nyerere.

Kwa upande wa msanii Juma Chikoka 'Chopa' akizungumza kwa uchungu alisema, "Agnes kafa namuona, tulikuwa tunaongea tunacheka, gafla akaniambia Chopa niitie nesi, nikatoka kwenda kumuita nesi, nesi anakuja akamtazama akaniambia kazi ya Mungu, amefariki.

"Binafsi sikutaka kuamini kwa wakati ule mtu naongea naye vizuri vipi uniambie amekufa, kuna mambo mawili makubwa Agness ameniambia ila nitaweka wazi baada ya msiba jamii ijue…

"Agness kafa kwa mambo mengi, pumu, kukaukiwa damu, vitu vingi, alikuwa anaumwa siku kama nne ndiyo alizidiwa akapelekwa kwa Mama Ngoma akaonekana ana hilo tatizo la kuishiwa damu…

"Nikapigiwa simu, familia yetu na ya Agness ni karibu mno, nikambiwa natakiwa kuchangia damu nikasema nipo tayari basi nikaenda lakini juzi (Alhamis) sikufanikiwa kutolewa, jana (Ijumaa) nikapigiwa simu niende nikatoe basi nikaenda, ndiyo nikawa naongea na Agness namwambia nimekuja kukutolea damu, akacheka…

"Akaniambia kaa hapa kwanza, basi nikakaa kwenye kitanda akaniwekea kichwa mapajani anacheka, nikawa namfariji tunaongea ndiyo mara akaniambia nenda kaite nesi kumbe ndiyo anakufa," alisema Chopa huku akibubujikwa machozi.

Chopa aliliambia Habari Leo kuwa Agness atakwenda kuzikwa Mbeya kwa baba yake na tayari mama yake mzazi alishatangulia mbele za haki.

Chanzo: habarileo.co.tz