Menu ›
Burudani
Tue, 26 Mar 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kampuni ya Alcor Life Extension Foundation ya Arizona, nchini Marekani inahifadhi miili ya watu waliofariki Dunia kwa kuiweka kwenye baridi kali, wakiamini kwamba kuanzia mwaka 2040, wataanza kuwafufua wafu hao kwa teknolojia ambayo wanaifanyia utafiti.
Kampuni hiyo imefanikiwa kufikisha idadi ya miili 200 huku watu wengine 1,000 wakiwa tayari wameshasaini mkataba kwamba wakifa wahifadhiwe na Kampuni hiyo.
Ili kupata fursa ya kufufuliwa teknolojia hiyo itapoanza kufanya kazi mwaka 2040, kabla ya kufa utalipia Tsh Milioni 470. Hata hivyo hakuna uhakika iwapo teknolojia hiyo itafanikiwa kweli.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live