Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mashindano ya Mitumbwi kufanyika Desemba 13 

E73a84def3e9f0817b9a6c9221d18737 Mashindano ya Mitumbwi kufanyika Desemba 13

Thu, 26 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MASHINDANO ya mbio za Mitumbwi mkoani Mwanza yanatarajiwa kufanyika Desemba13 mwaka huu katika ziwa Victoria.

Akizungumza na gazeti hili, Waandaji wa mashindano hayo ambae ni Meneja wa The Scope Solutions Herbert Rweikiza alisema jumla ya timu 40 za wanaume na wanawake ambao ni wavuvi kutoka wilaya za Ilemela, Nyamagana,Ukerewe,Buchosa na Sengerema

Rweikiza alisema mashindano hayo yatafanyika kufuatia juhudi zilizofanywa na Chama cha wapiga makasia Mwanza na Kampuni ya TBL kupitia kinywaji Cha Balimi Extra Lager.

"Mashindano ya mbio za Mitumbwi yatakuwa endelevu kwa kufanyika kila mwaka na yatakuja kujumuisha mikoa mingine kama vile Mara, Simiyu,Geita, Kagera na mkoa wa Kigoma kwenye ziwa Tanganyika na Tutaboreshwa na kuhusisha wadau wengi" alisema Rweikiza.

Alisema katika mashindano hayo zitatolewa zawadi kwa washindi wote wanaume na wanawake ambapo washindi wa kwanza watapata pesa taslimu 1,500,000 huku nafasi ya pili atachukua milioni moja na nafasi ya tatu atachukua 800,000 na nafasi ya nne atabeba 600,000

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya TBL Kanda ya Ziwa Issa Makani alisema wamejitokeza kudhamini michezo hiyo kwani wamekuwa wakifanya hivyo kwa kipindi Cha miaka 10 iliyopita.

Makani alisema kampuni yao inawathamini na kuwajali watu wa Kanda ya Ziwa na kwa vile mashindano ni mazoezi wataendelea kusaidia ili kujenga na kuweka miili ya watu katika hali nzuri ya ukakamavu.

Chanzo: habarileo.co.tz