Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashindano ya BSS yatua Dar, mamia wajitokeza

22091 Pic+BSS TanzaniaWeb

Sat, 13 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamia ya vijana wamejitokeza kwa wingi leo Ijumaa Oktoba 12, 2018 katika shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS) linaloendelea hivi sasa katika Ukumbi wa Nextdoor uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo ambayo kwa Dar es Salaam yanaanza rasmi leo, yanatarajia kupata washiriki 15 baada ya kupata sita kutoka mikoa mitatu.

Shindano hilo limeshapata washiriki kutokea mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza ambapo katika kila mkoa imepata sita huku kwa mkoa wa Dar es Salaam litasaka vipaji katika Ukumbi wa Next Door uliopo Oysterbay.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jaji Mkuu wa BSS, Rita Paulsen amebainisha kuwa mchakato wa kusaka vipaji mikoani ulikuwa wenye mafanikio makubwa kutokana na vijana wengi kujitokeza.

Amesema, vijana wamekuwa na hamasa zaidi ya kuimba na kuonyesha uwezo wao kwenye fani hiyo huku akibainisha kuwa majaji wenzake hawakuishia tu kuwapitisha walioimba vizuri ila hata wale waliochemka pia iliwapatia ushauri zaidi.

“Kusema ukweli hamasa imekuwa kubwa kwenye fani hii ya muziki, kitu nilichojifunza ni kuwa vijana wana nia ya dhati ya kutaka kujiendeleza kimuziki, na kuwa uwezo wao ni mkubwa ambao unapaswa kuendelezwa.

“BSS imekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana kuona mwanga kwenye fani ya muziki, kwa sasa tumejipanga kuhakikisha tunawainua na kuwafikisha mbali vijana wengi zaidi kwenye fani hii ya muziki,” amesema Madam Rita.

Amewataka washiriki kutoka Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi huku akibainisha kuwa majaji wamejipanga kutumia muda wao mwingi zaidi kusaka na kubainisha vipaji ambavyo ni lazima mshindi wa mwaka huu awe makini.

 

 

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz