Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wamshitaki Madonna

Madonna Afunguka Baada Ya Kulazwa Hospitali Madonna

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Pop kutoka Marekani, Madonna amefunguliwa mashitaka na mashabiki wake kutoka New York baada ya kuchelewa kupanda jukwaani katika tamasha lililofanyika Disemba mwaka 2023.

Mashabiki hao waliotambulika kwa majina Michael Fellows na Jonathan Hadden walifungua kesi ya madai ya mazoea mabaya na udanganyifu katika Mahakama ya Brooklyn wakieleza kuwa ‘tiketi’ za tamasha hilo ziliandikwa muda wa kupanda ‘stejini’ wa Madonna ni saa 2:30 usiku lakini alipanda saa 4:30 usiku.

Kufuatiwa na shauri lililopelekwa Mahakamani limeeleza kuwa Mashabiki hao wamedai kuwa walikumbana na changamoto kutokana na tamasha hilo kuchelewa kuisha zikiwemo kuchelewa kazini siku inayofuata na kupata gharama kubwa za usafiri wa umma baada ya tamasha hilo kuisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live