Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wamshambulia Sallam Sk kisa Harmonize

Harmo Na Sallam Mashabiki wamshambulia Sallam Sk kisa Harmonize

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na kile alichoandika Sallam Sk kuwa “Kwahiyo ameua lebo ameanzisha kundi na kujiita Mgambo mtu mbili” watu wengi wameunganisha ujumbe huo na Harmonize baada ya kuimba kuwa ametoboa kimuziki mbele ya Mkubwa Fella, Babu Tale, Kipara na Asake wa Tandale.

Baada ya ujumbe huo wa Sallam Harmonize alipost Insta Story yake na kuandika “Nikimkata” halafu akacheka.

Mashabiki hawajakaa kimya, wamemjia juu Sallam Sk wakiamini ujumbe huo unamhusu Harmonize na wengi wao wakimwambia Sallam anajishusha kumjibu Harmonize sio level zake.

Wengine wamefurahishwa na kusema kuwa kumbe Sallam anasikilizaga nyimbo za Harmonize na kumkaribisha Konde Gang wakimuita shabiki namba moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live