Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wamshambulia Rihanna kwenye sherehe ya mtoto wa bilionea

Rihanna Msz Mashabiki wamshambulia Rihanna kwenye sherehe ya mtoto wa bilionea

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rihanna ameshutumiwa kwa kufanya “bare minimum” kwenye sherehe ya harusi ya familia ya mabilionea nchini India Jumamosi usiku.

Daily Mail iliripoti kwamba mwimbaji huyo alilipwa dola milioni 6.3 kwa hafla hiyo ilyofanyika kabla ya harusi kamili huko Gujarat iliyoandaliwa na bilionea Mukesh Ambani kwa ajili ya mwanawe Anant, ambaye anafunga ndoa na Radhika Merchant huko Mumbai mnamo Julai.



Miongoni mwa wageni 1,200 zaidi walikuwa Mark Zuckerberg, Ivanka Trump, na nyota wa Bollywood Shah Rukh Khan, Ranveer Singh, Anil Kapoor, Amir Khan na Deepika Padukone.

Rihanna alitumbuiza vibao kama vile "Umbrela", "Work" na "Diamond". "Shukrani kwa familia ya Ambani niko hapa usiku wa leo kwa heshima ya Anant na Radhika. Asante kwa kuwa nami hapa. Mungu abariki umoja wenu. Nawatakia kila la kheri. Hongera,” mwimbaji huyo aliyegeuka kuwa mjasiriamali alisema, kulingana na Post.

Miezi kadhaa kabla ya harusi, familia tajiri nchini India kwa kawaida hupanga karamu kubwa, chombo hicho kiliripoti, na kuongeza kwamba sherehe hizo mara nyingi hugharimu zaidi ya dola milioni 150.

Rihanna alivalia gauni la kijani na waridi lililokumbatia mwili kwa ajili ya onyesho lake kwenye karamu ya harusi lakini mashabiki hawakufurahishwa, wakielezea tamasha lake kama "kuchosha".

"Alipata sarafu hiyo na kusema f-k y'all ima fanya niwezavyo", mtumiaji mmoja wa X alisema.

"Nimekuwa nikisema kwamba yeye ni msanii mvivu sana ... hajawahi kuchukua muda kuboresha kazi yake," mwingine aliandika.



Rihanna, ambaye alitajwa kuwa "Mwanamuziki tajiri zaidi wa kike" na Forbes mnamo 2021, alikuwa hajaonekana kwenye jukwaa kwa takriban miaka minane. Mmiliki wa biashara wa Fenty na sasa mama kwa watoto wawili wa kiume pamoja na mwanamuziki mwenzake A$AP Rocky, hata hivyo huenda wakaachia ngoma mpya hivi karibuni.

Mwezi uliopita, Rocky alipokuwa akipiga picha ya selfie na shabiki huko Paris kama inavyoonekana kwenye video kwenye X, mtu alisikika akimuuliza amwambie Rihanna kwamba mashabiki hawawezi kungoja aachie albamu mpya. "Anaifanyia kazi," Rocky alijibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live