Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Mobeto, Uwoya waibua mapya

11814 Mobeto+pic TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Saa kadhaa baada ya Hamisa Mobeto na Irene  Uwoya kutekeleza agizo la kuomba radhi kwa kuweka picha za utupu katika mtandao wa kijamii wa Instagram, mashabiki wa mastaa hao wameibua mapya.

Wengi waliotoa maoni kwenye ukurasa wa Hamisa wameonyesha kushangazwa na uamuzi huo kuchukuliwa sasa wakati picha zake, ameziweka takribani mwaka mmoja uliopita.

Wasanii hao leo Alhamisi Julai 19, 2018 wametakiwa na kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano (TCRA)  kuomba radhi kwa kuweka picha hizo, jambo ambalo wamelitekeleza kupitia kurasa zao za mtandao huo.

Mashabiki hao walikwenda mbali  zaidi na kuhoji nini hatima ya tasnia ya mitindo kama wana mitindo watakuwa wanazuiwa kupiga picha na baadhi ya mavazi.

Mashabiki wa Hamisa waliopo Kenya walimshauri mrembo huyo kuhamia nchini kwao kwa kile walichodai hakuna sheria hizo.

Kwa upande wa Uwoya, mashabiki wengi walionyeshwa kushangazwa na picha iliyotumika kuomba radhi.

Picha hiyo ambayo inaacha wazi sehemu ya mapaja na miguu imetafsiriwa kama mwendelezo wa picha za ajabu.

Shabiki mmoja aliandika," Sasa hapo ndio umeomba radhi ya nini wakati umeweka tena picha ya kututega, kamuombe radhi mumeo,".

Wapo pia ambao walimpa moyo na kumtania kuwa role model wake ambaye ni Beyonce ndiye kamponza.

Chanzo: mwananchi.co.tz