Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Beyoncé wagawanyika kutokana na onyesho la Dubai Atlantis Royal

Beyonce Mgawanyiko Mashabiki wa Beyoncé wagawanyika kutokana na onyesho la Dubai Atlantis Royal

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Beyoncé amerejea jukwaani kwa onyesho lake la kwanza la moja kwa moja katika miaka mitano - lakini sio kila mtu aliyefurahiya.

Mwanamuziki huyo wa Marekani aliongoza tamasha la kibinafsi huko Dubai kuashiria ufunguzi wa hoteli ya kifahari ya Atlantis The Royal.

Licha ya sera kali ya kutotumia simu kwenye tamasha la kipekee, lenye viti 1,500, picha za kipindi hicho zilifurika mtandaoni.

Mashabiki wengi walifurahi kuona kurejea kwa Queen B, lakini wengine hawakufurahi kwa sababu Dubai ina sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Renaissance, albamu yake ya hivi punde zaidi, imeadhimishwa kwa "kuheshimu utamaduni wa watu weusi" na kupata msukumo kutoka kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Inatoa heshima kwa muziki wa dansi ulioibuka kutoka kwa jamii ya wapenzi wa jinsia moja.

Kwa hivyo baadhi ya mashabiki wamekosa raha kwamba mwimbaji huyo amefanya onyesho la moja kwa moja katika taifa ambalo halitambui haki za LGBT.

Dubai ni sehemu ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kundi la mataifa ya Mashariki ya Kati yanayofuata sheria kali na yenye sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Qatar iliyo karibu, ambayo iliandaa Kombe la Dunia la 2022, ina sheria sawa na hizo.

Ilikosolewa kwa mtazamo wake kwa watu wa LGBT, rekodi yake ya haki za binadamu na jinsi inavyowatendea wafanyakazi wahamiaji.

David Beckham alipingwa vikali hasa na mcheshi Joe Lycett - kwa kutia saini mkataba wa pesa nyingi na serikali ya Qatar ili kutangaza tukio la Kombe la Dunia.

Nyota wa Uingereza Kitty Scott-Claus aliuliza kama kuna "sheria nyengine kwa mmoja na tofauti kwa mwingine", akirejelea upinzani dhidi ya Beckham.

Chanzo: Bbc