Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki na mbwa kuungana mtaani mazishi ya mchekeshaji

Mashabiki Na Mbwa Kuungana Mtaani Mazishi Ya Mchekeshaji Mashabiki na mbwa kuungana mtaani mazishi ya mchekeshaji

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mazishi ya Paul O'Grady yatafanyika katika nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Kent nchini Uingereza baadaye, huku mashabiki wake wakiwa tayari kujipanga kwenye msururu pamoja na mbwa mitaani kutoka kituo cha mbwa cha Battersea Dogs & Cats Home.

Mchekeshaji huyo na mtangazaji, aliyefariki wiki iliyopita, akiwa na umri wa miaka 67, atazikwa katika ibada itakayohudhuriwa na watu wachache katika kitongoji cha Aldington.

Linatarajiwa kufanyika gwaride la heshima la mbwa kutoka katika nyumba ambako alifanya msururu wa vipindi vya televisheni unaofahamika kama For The Love of Dogs (Kwa mapenzi ya Mbwa).

Mchezaji filamu na rafiki yake Michael Cashman alisema:

"Moyo wangu utakuwa unaomboleza, lakini nitakuwa ninatabasamu kuhusu upendo na raha."

Chanzo: Bbc