Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Nigeria wairipoti Akaunti ya Grammy

Grammy Account .jpeg Mashabiki Nigeria wairipoti Akaunti ya Grammy

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ugawaji wa Tuzo kubwa za Grammy kuwatosa Ma-staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, mashabiki kutoka nchini humo wamechukizwa na kitendo hicho na kuamua kui-report 'akaunti' ya Instagram ya Grammy huku wakidai kuwa hawakutenda haki kwa wanamuziki hao.

Kufuatiwa na video zinazoendelea kusambaa mitandaoni zimewaonesha vijana hao wakiwa na simu zao waki-report ‘akauti’ hiyo kutokana na wasanii waliowatarajia kuondoka na ushindi mnono, kushindwa kuchukua tuzo hizo.

Ma-staa ambao walifanikiwa kutajwa katika vipengele kadhaa kwenye tuzo hizo ni Burna Boy, Davido, Asake na wengineo lakini wote hao hawakuweza kuondoka na tuzo yoyote siku hiyo.

Tuzo za Grammy zilitolewa usiku wa kuamkia jana Februari 4, nchini Marekani katika ukumbi wa ‘Crypto’.

Tazama Video hapa chini;

View this post on Instagram

A post shared by Mwananchi Scoop (@mwananchiscoop)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live