Mrembo asiyeishiwa vituko kwenye mitandao ya kijamii, Masha Love amesimulia jinsi alivyomtia vichwa Jimmy Mafufu baada ya kumzingua kuhusu ujauzito alionao.
Akizungumza kwenye kipindi cha Lavidavi cha Wasafi FM, Masha alisema alipopata mimba ambayo ni ya miezi miwili, alipomwambia Jimmy alimblock namba zake na ndipo alipomkutana naye mahali kumkata vichwa.
“Nilikuwa kwenye gari nyuma la Juma Lokole, Juma akamuita mimi nikiwa siti ya nyuma, alipotaka kuchungulia nyuma niliko nilifungua kioo nkatokea dirishani na kumkata vichwa vya maana mpaka akavimba kwenye uso ndipo tukaamuriwa,” alisema Masha.
Masha anasema amekaa na Jimmy kwenye mahusiano kwa kipindi cha miezi nane lakini hata hivyo, Jimmy amekanusha kuwa na uhusiano naye.