Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masha Love amvaa Jackline Wolper

Masha Lovers Masha Love amvaa Jackline Wolper

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Movies, Masha Love amesema tangu Jackline Wolper akatae kumrudishia pesa zake alizomtunza kwenye harusi yake, amemchukia kiasi cha kumlaani.

Masha ambaye amekuwa aki-trend kwa kuwachachafya mastaa wenzake, amesema tangu amjibu maneno ya shombo, maisha ya Wolper yamezidi kudorola kiasi cha kuomba kazi kwa makampuni badala kazi kumfuata.

Masha amesema siku hizi Wolper anaomba matangazo kutokana na kuishiwa pesa, huku yeye akizidi kung'aaa na mpaka sasa yeye ndiye mwanamke Staa anayeongoza kwa kupewa balozi nyingi na makampuni mbalimbali.

Pia, Masha amesema amegundua Wolper ni m'beya na mnafiki wa kupindukia wa kuyatoa maneno Mbagala na kuyapeleka Kinondoni ilimradi tu watu wagombane.

Ameapa kutokumsamehe na amemlaani katika maisha yake yote, ambapo amesema laana hiyo itaendelea kutafuna maisha ya Wolper na kwasasa hazitaki hizo pesa ameamua kumuachia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live