Wakati sakata la katibu wake kufariki na kuhusishwa na mkewe likiendelea kutikisa kwenye mitandao ya kijamii, mchekeshaji na mchungaji Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ametoa kauli inayoonekana inahusu sakata hilo.
Kwa siku kadhaa sasa, sakata la aliyekuwa Katibu wa Kanisa la Masanja kufariki na kuacha ujumbe kwenda kwa Monica (mke wa Masanja) akidai ni mwanamke wake na alimpa faraja ya moyo na kamwe hatamsahau.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, leo Oktoba 06, 2022 Masanja ameandika:
“Sehemu kubwa ya kizazi chetu inapenda kushabikia umbea, ugomvi & controversies sababu ni mambo yanayotrendi/kushughulisha. Tatizo ni kwamba hayo mambo hayadumu na hayajengi so ili kukidhi kiu muda wote watu wanajichosha kuyatafuta. Mungu atusaidie tutafute yanayodumu na kujenga.”