Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masanja: Waambieni wachungaji wenu wavae jinzi

Masanja Masanja: Waambieni wachungaji wenu wavae jinzi

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchekeshaji na mchungaji Emmanuel Mganya ‘Masanja Mkandamizaji’ amewataka wale watu ambao wana mashaka na uchugaji wake, wawaambie wachungaji wao wavae na kuwa kama yeye.

Masanja amefunguka hayo baada ya kubanywa na waandishi wa habari hivi karibuni ambao walimuuliza maswali mbalimbali likiwemo hilo la kwamba baadhi ya watu hawana Imani na uchungaji wake.

Masanja alisema ameamua kuwa mchungaji wa aina yake sasa wasimfananishe na wachungaji wao wanaowafahamu.

“Waambieni wachungaji wenu wawe kama mimi, mnapotaka mimi nifanane na wao ni upendeleo. Waambie wavae jinzi twende kazi,” alisema Masanja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live