Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Martin Kadinda aja kivingine, sasa mbugani

Kadinda.jpeg Martin Kadinda akiwa katika moja ya maonesho ya mitindo

Thu, 27 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunifu nguli wa mavazi hapa nchin Martin Kadinda, anatarajiwa kutambulisha collection yake Mpya mavazi Aliyoipa Jina la Escapade katika onyesho la ubunifu wa mavazi lenye dhima ya kuhamasisha utalii mkoani Manyara katika hoteli ya Mawe mawe Januari 29.

Hii itakuwa ni onyesho lake la kwanza kwa mwaka huu kushiriki hapa nchin mara ya mwisho alitambusha collection ya Vanguard, katika tamasha la Swahaili Fashion Week 2020.

Akizungumza na ukurasa huu amesema dhumuni la Escapade collection ni kushawishi watanzania kufanya utalii wa ndani wakienda mbugani katika mavazi yanayo kwenda na wakati.

"Tanzania tuna vivutio vingi ndani ya miaka miaka miwili tumepata muamko mzuri wa kutembelea vivutio vyetu ila wengi wamekuwa wakipata shida katika upande wa mavazi ndio maana nimebuni Escapade collection ambayo ni mwendelezo wa collection yangu ya mwaka 2020 Vanguard , kwa ajili ya kuleta umaridadi wakati wa safari za utalii wa ndani," anasema Martin Kadinda.

Aliongeza kuwa kabla ya onyesho hilo kesho atashiriki kuuza vifaa mbalimbali alivyo tengeneza vinavyotumika katika safari za utalii katika mnada utakaofanyika katika hoteli ya Mawe mawe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live