Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mark Zuckerberg: Ilikuwa ninunue Twitter hata kabla ya Elon musk

Mark Zuckerberg Mark Zuckerberg.

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmiliki wa mtandao wa META, ndugu Mark Zuckerberg kwenye mahojiano yake na mtandao wa 'verge' amefunguka kwa kusema kabla ya kununuliwa na Elon Musk.

Moja kati ya vitu ambavyo aliwahi kuzungumza na mmlikiwa wa mtandao 'Twitter' zamani 'X' kwa sasa Bwana Jack Dorsey ni kuhusiana na yeye kununua mtandao huo.

"Niliwahi kuwa na mazungumzo na Jack kuhusu hilo kabla ya kutoka kwenye nafasi yake ya awali, lakini nadhani kila mjasiliamali yuko na malengo ya tofauti.

"Kwa sasa Elon ni kama wakala wa mabadiliko tangu amenunua amebadilisha baadhi ya vitu kwenye mtandao huo, binafsi naweza kuwa na matumaini kidogo au nadhani kuna nafasi ndogo sasa kuliko ilivyokuwa hapo awali."

Mark amejaribu kuweka wazi kwamba aliwahi kuwa na mpango wa kununua mtandao huo lakini baada ya Elon Musk kununu mtandao huo, hali ikawa tofauti kiasi cha kuhisi hatoweza tena kununua mtandao huo kwani nafasi ya yeye kununua mtandao huo kwa sasa ni ndogo ukilinganisha na kipindi unamilikiwa na Jack Dorsey.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live