Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo kutua Konde Gang au Kings Music?

MARIOO Marioo kutua Konde Gang au Kings Music?

Mon, 11 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja kati ya jina ambalo linatajwa na mashabiki, kuhusu kusainiwa kwenye lebo ya Kings Music Records ya Alikiba au Konde Gang ya Harmonize basi ni Marioo.

Wote tunajua kwamba lebo ya Kings Music Records, imeondokewa na wasanii wawili ambao ni Cheed na Killy na lebo ya Konde Gang imeanza na msanii wake mpya Ibraah Tz.

Sasa kuhusiana na jina lake kutajwa sana kwenda kwenye hizo lebo mbili, msanii Marioo mwenyewe amefunguka kusema "Sio kitu kibaya kwa sababu ni watu ambao wanasapoti muziki vizuri na kuna vijana kule wapo, watu kuniongelea mimi kuhusu kwenda sehemu hizo sio kitu kibaya sana, lakini binafsi mimi mwenyewe sina mpango wa kusainiwa lebo yoyote kwa sasa hivi sana sana hapa Bongo".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live