Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo 'kumwakilisha' Harmonize Wasafi Festival

Marioooo Harmo Marioo 'kumwakilisha' Harmonize Wasafi Festival

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Omary Ally Mwanga 'Marioo' amefunguka kuwa moja kati ya nyimbo ambazo anazitegemea sana ni kolabo yake na Harmonize #Naogopa.

Marioo amesema kuwa ni lazima itasikika kwenye jukwaa la Wasafi Festival Mtwara itakayoanza kutikisa mwezi ujao wa Septemba akiwa ni miongoni mwa wasanii walioorodheshwa kufanya shoo kwenye Tamasha hilo chini ya diamond Platnumz.

“Lazima ni-perform kwa sababu ni moja ya ngoma zangu ninazozipenda zenye mahadhi ya Bongo Fleva, kwa nini nissimbe? Lazima ni-perform 'Naogopa', tena naweza kuanza nayo, nikachukua kile kijiji chenyewe cha Mmakonde halafu nikaendelea na shughuli zangu nyingine,” amesema Marioo.

Kauli hiyo ya Marioo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Harmonize kusema kuwa hatoweza kufanya shoo kwenye Tamasha hilo lakini atawasapoti Wasafi kwa namna nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live