Staa wa Bongo Fleva, Omary Ally Mwanga maarufu kama Marioo kakiri kwamba yupo tayari kulipa mahari ya Tsh milioni 100 kwa mpenzi wake ambaye pia ni sosholaiti Paula Kajala.
Penzi la wawili hao kwa sasa limefikia patamu ikiwa ni miezi saba toka walipoanza kudeti. Akifanya mahojiano hivi majuzi na runinga ya East Africa TV, Marioo alikiri kukoshwa na Paula kiasi cha kuwa tayari kumlipia kiasi hicho kama mahari.
Paulah ni binti ya produsa maarufu na mkongwe P Funk Majani pamoja na mwigizaji soshiolaiti Fridah Kajala. Binti yao huyo aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mwanamuziki Rayvanny. kabla ya kuwa na Marioo wake.