Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo hajanisaidia - Abby Chams

Marioo Abby Chams Ers.jpeg Marioo hajanisaidia - Abby Chams

Sat, 30 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Abigail Chamangwana 'Abby Chams' amesema kuwa msanii wa Bongo Fleva, Omary Ally Mwanga maarufu kama Marioo hana washauri wazuri hasa kwenye kuchagua kipi cha kuzungumza hadharani na kipi si cha kuzungumza.

Abby Chams amesema hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Alfred Bundala wa SNS kufuatia wawili hao kupishana mitandao kisa kikidaiwa kuwa Marioo kufuta verse ya Abby kwenye ngoma yake ya Love Song.

“Nilimshangaa pia kusema amenisaidia baada ya kufanya nae ngoma yangu ya 'Nani', muziki ni biashara, wanamuziki wawili wamekutana wamelipwa na wamefanya kazi. Yeye alilipwa royal tizzy and publishing, hata akisoma mkataba wake aliopewa na Sonny.

“Labda angepata mwanasheria amsaidie kusoma na kuelewa mkataba ule lakini anajua amelipwa na ni biashara kwa hiyo sote tulisaidiana. Ule wimbo uliingia number 1 trending. Marioo ni msanii anayetoa nyimbo kila siku lakini sijawahi kuona wimbo wake umeenda trending namba 1 ndani ya saa 24.

“Ni wimbo wa kwanza kutoka Tanzania ambao uliingia kwenye Daddy Show kwenye Apple Music, jambo ambalo ni kubwa sana kidunia. Haya yote yalifanywa na Sonny kwa ajili yangu na si yeye, kwa hiyo asiseme kwamba alinisaidia. Hii ni Sanaa haya mambo wakati mwingine yanatokea, namwachia Mungu," amesema Abby Chams.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live