Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo atumia mamilioni kutengeneza nyimbo

D0662127f941963c9ee5f8101f8d3a01 Marioo atumia mamilioni kutengeneza nyimbo

Sun, 29 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Omary Mawanga 'Marioo' amesema ametumia Sh milioni 30 kutengeneza nyimbo sita za audio na video zake.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Marioo alisema hiyo ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu kutumia fedha nyingi Ili kutengeneza kazi zenye ubora, ambazo zitawavutia wengi.

"Kwanza nimefanya video sita na audio kibao nimerekodi wakati wa kutoka ukufika watazisikia, na hii video ambayo nimeitoa sasa hivi nimetumia milioni 30 kuishoot kwa hivyo nimefurahi kwasababu ilikua ni ndoto yangu kufanya video nzuri," alisema.

Alisema kazi hizo ikiwemo hiyo video aliyopanga kuachia wakati wowote endapo mambo yatakaa sawa inavionjo tofauti, ambavyo mashabiki wake wote watakuwa na wakati mzuri wa kuburudika.

Marioo nyota anayetamba na nyimbo kadhaa, ikiwemo Inatosha ni miongoni mwa wasanii wanaokuja kwa kasi kwenye soko la muziki huo ambao unazidi kujikusanyia mashabiki wengi.

Chanzo: habarileo.co.tz