Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo apelekwa mahakamani

Mariooo.jpeg Marioo apelekwa mahakamani

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Omary Mwanga "Marioo", amefunguliwa kesi ya madai na Kampuni ya Kismaty kwa madai ya kuvunja mkataba wa kutumbuiza kwa kutoonekana kwenye hafla ya Mr & Miss vyuo vikuu Kanda ya Kaskazini.

Kulingana na madai yaliyowasilishwa Mahakama Kuu Masjala ya Wilaya ya Arusha mbele ya Jaji Joackim Tiganga imeelezwa Marioo na Meneja wake, Sweetbert Mwinula wanakabiliwa na tuhuma za kuvunja mkataba huo wa Septemba 23, 2021, wakidaiwa jumla ya Tsh. 550,000,000.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa Mahakama Kuu mnamo Machi 18 na 19, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live