Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo: Video ya Diamond na Mimi Mars iliniumiza

Mimi Mars Diamond .jpeg Diamond Platnumz na Mimi Mars

Sun, 22 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marioo; ni staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania ambaye kwa mara ya kwanza amefungukia ile video ya mrembo anayedai ni rafiki yake, Mimi Mars na kaka mkubwa, Diamond Platnumz.

Kama utakumbuka, video ya Mimi Mars ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Diamond iliyowaonesha wakijiachia kwenye bwawa la kuogelea nyumbani kwa Diamond na kuzua maneno mengi kwamba huwenda kulikuwa na wimbo wanaachia, lakini miaka imekatika hakuna cha wimbo wala video.

Sasa; Marioo ambaye kuna tetesi kwamba anaminya kimapenzi na Mimi Mars amefunguka juu ya video hiyo baada ya kuulizwa ni jambo gani lililowahi kumuumiza kwenye maisha yake ambapo majibu ni haya;

“Yapo mengi ila nilipoonaga ile clip video ya rafiki yangu wa kike (Mimi Mars) akiogelea kwenye pool na bro (Diamond) ilinigusa nayo ile…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live