Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo: Najuta kumsaidia Abby Chams

Marioo Abby (11).jpeg Marioo: Najuta kumsaidia Abby Chams

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Toto Bad Marioo amefunguka mwanzo mpaka mwisho kilichotokea kwenye Wimbo wa Love Song na kusema kuwa Abby Chams aliukataa wimbo na Kusema mbaya hivyo yeye akaamua kumtafuta Alikiba kwa ajili ya Collabo hiyo.

“Najutia kabisa kumsaidia kwa sababu kama jana nasoma kwenye comment watu wanasema tumemuonea, watu wanamtukana girlfriend wangu, hawawezi watu kumtukana mpenzi wangu kwa sababu ya kipaji change mwenyewe.

“Ukizungumzia hiyo ngoma ambayo nimefanya na Alikiba ni wimbo wangu, sijamwandikia ngoma moja nimemwandikia nyingi tu na nyingine hazijaisha.

“Kuna siku nilikuwa naye nikamwambia nimetengeneza ngoma moja kali ya mapenzi naona kama ukiimba kiwswahili vizuri itakusaidia. Tatizo lake anaweza akasikia kitu kizuri lakini yeye mwenyewe asijue kama ni kizuri au asikipende.

“Alijaribu kuimba lakini mwisho wa siku akasema hawezi kwa sababu imekaa Kiswahili sana, nikamwambia aachane nayo nitamtafutia nyingine. Sikumuita studio tufanye ngoma tayari nilikuwa nimeshafanya ile ngoma na zipo nyingi.

“Kusema kweli ana kipaji sana lakini sasa hivi amekuwa akipenda kiki na trend za kwenye mitandao ambazo hazina msaada wowote kwake, anaona anavyotrend inamtengenezea kitu kumbe inamharibu, kipaji chake ni zaidi hata ya hivyo vitu anavyofanya,” amesema Marioo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live