Msanii wa Bongo Fleva, Omary Ally Mwanga maarufu kama Marioo amesema kuwa ameshakabidhiwa mpenzi wake Paula kutoka kwa mama yake Kajala hivyo sasa ana amani ya moyo.
Marioo na paula wanatajwa kuwa ni wapenzi na wamekuwa wakionekana katika mazingira ya kimahaba mara kwa mara.
"Upendo ambao naupata kutoka kwa mama mkwe ni mkubwa sana, tumeshaongea vitu vingi mimi na mama yangu, tumeshapanga vitu vingi sana. Mimi niseme tu nampenda sana na Mungu amfanyie upesi mambo yazidi kuwa mazuri.
“Nafurahi kwamba kanikabidhi mtoto, japo sio rasmi lakini, nimefurahi, nashukuru nampenda sana mama yangu, Mungu akubariki," amesema Marioo.