Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo: Kufanya kolabo na wasanii wakubwa ni changamoto

Mariooooooo Marioo

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongofleva, Marioo amesema kuna wasanii wakubwa kufanya nao kazi ni changamoto kutokana na kutotaka mapendekezo.

Marioo ametoa kauli hiyo wakati akimshukuru Barnaba kwa kumshirikisha katika albamu yake, Love Sound Different.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Barnaba ameandika; "Nashukuru sana kaka yangu Barnaba kwa kunipa nafasi ya kuwa kwenye Album yako, Love Sound Different.

"Lakini pia asante kwa kuskilza wazo langu kwenye hii project Maana kuna baadhi ya kaka zetu wengine wakikutumia wimbo wanataka ufanye huo huo hata kama hujapenda na ukisema bro naomba tufanye wimbo mwengine wanaona kama umewatusi.Lengo langu kufanya wimbo pendwa kwenye Album yako na nashukuru Mungu limetimia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live