Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapya yaibuka kesi ya mauaji ya Takeoff

Skynews Takeoff Migos 5950734 Mapya yaibuka kesi ya mauaji ya Takeoff

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmililiki Wa Eneo Alikouawa Rapa Takeoff “810 Billiards & Bowling” Huko Houston, Texas Ameiomba Mahakama Ifutilie Mbali Kesi Inayomkabili Ya Kwamba Eneo Lake Ni Moja Ya Sababu Ya Kifo Cha Takeoff.

‘810 Billiards & Bowling’ Wamekanusha Kuhushika Na Chochote Kibaya Katika Kifo Cha Takeoff Huku Wakitupa Lawama Kwa Mshukiwa Wa Mauaji Ya Takeoff ‘Patrick Clark’ Ambaye Yupo Jela Kwa Sasa Na Wengine Akiwemo Takeoff Aliyekuwa Akicheza Kamari ‘Mchezo Wa Kete’ Na Wenzake Eneo Hilo

Kumbuka Juni Mwaka Jana 2023 Mama Mzazi Wa Marehemu Takeoff “Titania Davenport Alienda Mahakamani kumshtaki mmiliki wa eneo la Houston ‘810 Billiards & Bowling’ ambalo Takeoff alipigwa risasi Na Kuuawa

Kwenye mashtaka hayo, Mama Takeoff alidai kwamba, eneo hilo lilishindwa kuweka ulinzi wa kutosha pamoja na vifaa vya kubaini silaha ndani, hivyo aliwashtaki kwa uzembe. Na Alidai Anahitaji kulipwa fidia chini ya sheria ya Texas kwa madhara ambayo ameyapata ikiwemo ya Kiakili, maumivu na kukosa kipato. Fidia Ya Kiasi Cha $1M Zaidi Ya Tsh Bilioni 2.3/=

Chanzo: www.tanzaniaweb.live