Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Mapya yaibuka aliyefariki akifanya upasuaji

Melissa Kerr Mapya yaibuka aliyefariki akifanya upasuaji

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa wa Uingereza na Uturuki watakutana kujadiliana kuhusu mfumo wa udhibiti kufuatia kifo cha Mwanamke mmoja mwaka 2019 kilichotokana na upasuaji wa kuongeza makalio.

Melissa Kerr alifariki dunia jijini Istanbul mara baada ya kufanyiwa upasuaji uliohusisha kukusanya mafuta na kuyaweka kwenye makalio yake.

Kifo cha Melissa (31) kilitokana na mafuta aliyochomwa kwenye makalio kuingia kwenye mshipa na baadaye kwenda kuziba ateri ya mapafu.

Sababu ya kifo chake ilirekodiwa kuwa ni kuziba kwa ghafla kwa mishipa ya damu kulikotokana na kuwekewa mafuta. Huku sababu kuu ikiwa ni upasuaji wa urembo.

Maafisa hao wameeleza kuwa Melissa hakuwa amepewa taarifa za kutosha kuhusiana na hatari za upasuaji huo ikiwemo kiwango cha vifo.

Vilevile wamesema yawezekana hakuna kabisa udhibiti au upo kidogo sana kuhusiana na upasuaji wa urembo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza imeeleza kuwa inazo taarifa za zaidi ya raia wake 25 waliopoteza maisha nchini Uturuki tangu Januari 2019 baada ya kufanyiwa upasuaji wa aina mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live