Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mapenzi ya mastaa na visa vyao

Manara Zaylissa Ms Manara na Zaylissa.

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtaani wanasema Tanzania ukifa na 'stresi' ni uzembe wako mwenyewe, kwani vipo vitu vingi vinavyoweza kukupa furaha ya kukusahaulisha changamoto za hapa na pale kwa muda wakati unafikiria namna nzuri ya kuzitatua.

Kwenye upande wa burudani, hasa wasanii wa Bongo Fleva, Bongo Movie ama watu maarufu wa mitandaoni, wanapoingia kwenye mapenzi hasa yakiwa mapya, kama huna mwenza unaweza ukatamani kutafuta, au ukiwa naye unaweza ukaona labda hamjayajuliana namna ya kutamba nayo kwenye jamii.

Ajabu sasa mapenzi yao yamekuwa hayadumu wakati mwingine kuzalisha chuki baina yao, ingawa hakuna chuki wala furaha inayodumu.

Tunakuletea uhusiano wa mastaa wanao-trend kwenye mitandao ya kijamii kutokana na wanavyoishi maisha ya mitandaoni. Je, ni uhusiano gani unaokuvutia zaidi?

MANARA & ZAYLISA

Penzi la Haji Manara, msemaji wa zamani wa Simba na Yanga, ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ndilo linalotamba kwenye mitandao ya kijamii baina yake na Zaylisa ambaye ni muigizaji wa tamthilia ya Jua Kali.

Zaylisa anayeonekana kutupiana vijembe na mtalaka wa Manara, anayejulikana kwa jina la Rushayna. Kama haitoshi Zaylisa kwa sasa nyota yake inang'ara na ameanza kupata matangazo mbalimbali ya kumuingizia pesa.

MARIOO & PAULA

Wakati penzi kati ya nyota wa Bongofleva, Marioo na Paula, ambaye ni mtoto wa masupastaa, Kajala Masanja na Prodyuza P-Funk 'Majani' lilipoanza, watu waliona binti huyo ni kama alikuwa analipa kisasi cha kuachana na Rayvanny.

Sasa penzi hilo limekolea na wawili wanaonyeshana mahaba moto moto na kupeana zawadi za hapa na pale mbele ya mashabiki wao wanaowafuatilia kwenye mitandao ya kijamii.

JUX & KAREN

Uhusiano wake ambao ulikuwa umebamba zaidi ni baina yake na Vanessa Mdee, hadi kuachana kwao haikuwa rahisi kwa mashabiki wao kuamini.

Venessa akaamua kuwaonyesha mashabiki kwa vitendo, baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya, Rotimi, muigizaji nyota wa Kimarekani mwenye asili ya Nigeria, aliyezaa naye watoto wawili.

Kwa upande wake, Jux ambaye aliwahi kufanya wimbo kwa kushirikiana Vanessa Mdee ulioitwa 'Juu' ambao ulifanya vizuri sokoni kwa wakati huo, yeye tangu aachane na mrembo huyo amekuwa akionekana na warembo tofauti na kwa nyakati tofauti, ila kwa sasa katulia na mlimbwende Karen Bujulu.

DIAMOND & ZUCHU

Supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametoka na warembo wa kila aina, kuna wakati mwingine walikuwa wakirushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii.

Penzi ambalo lilitamba kila kona lilikuwa kati yake na Wema Sepetu likaja kuzimwa na Zari Hassan 'Zari The Boss Lady' ambaye ni mama watoto wake wawili, likaingia dosari baada ya Hamisa Mobetto kuingilia kati, hata hivyo, na yeye mwanamitindo huyo akatafutiwa mwenzake Tanasha Donna, hao pia ni mama watoto wake.

Wanawake hao aliozaa nao aliwashirikisha kwenye nyimbo zake, Zari alionekana kwenye video ya Utanipenda, Hamisa alikuwa video Queen kwenye wimbo wa Salome, Tanasha alishirikiana naye kwenye wimbo wa Gere na Zuchu kaimba naye Mtasubiri ambaye kwa sasa ndiye yupo naye penzini.

BILLNASS & NANDY

Penzi lao lilianza kama utani hadi kufikia kufunga ndoa na sasa wamejaaliwa kupata mtoto wa kike, ukiachana na mapenzi, wawili hao wanashirikiana kufanya ngoma kali kama Bugana, Bye na Do Me.

WHOZU & WEMA

Wakati penzi lao linaanza watu waliona kama kiki, ilitokana na Wema Sepetu kuwafanyia mahojiano Whozu na mzazi mwenzake Tunda (mama Lola).

Kadri siku zinavyoendelea penzi lao limekuwa zito, huku Wema akionekana kutoa sapoti kubwa kwenye mziki wa mpenzi wake Whozu.

Moja ya mambo ya kukumbukwa ni pale mama mkwe wa Whozu yaani mama Sepetu alipomchana kijana huyo kwamba anakaa tu kwenye nyumba ya Wema, wakati wa sherehe ya bethidei ya Wema. Whozu alitaniwa sana na watu mitandaoni wakiwamo wasanii wenzake waliodai kwamba watamchangia pesa ili apate nyumba ya kuishi kama ameshakataliwa na mama mkwewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live