Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mapacha Walioungana Viwiliwil, Utashangaa Maisha Yao

Mapacha (2).jpeg Mapacha

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HAYA kweli ni maajabu ya Mungu! Mapacha wawili nchini Marekani Abigail Hensel (Abby) na Brittany Hensel ambao wameungana viwiliwili vyao tangu kuzaliwa Machi 7, 1990 wakiwa na mwili mmoja lakini kila mtu ana kichwa chake, moyo wake, tumbo lake , uti wa mgongo na hata mapafu yake pia.

Abby na Brittany kila mmoja ana mguu mmoja na mkono mmoja ambayo inafanya kazi kwa kushirikiana, kwa hiyo hushirikiana wakati wa kutembea, kupiga makofi, kuogelea, kukimbia, kuendesha Gari n.k ingawa wana uwezo wa kuongea, kula au kuandika kila mtu anafanya kivyake.

Walizaliwa New Germany, Minnesota Marekani wakasoma hadi Elimu ya Chuo Kikuu, Bethel University na sasa wameajiriwa kama walimu wakifundisha Sunnyside Elementary, New Brighton.

"Kwa sasa tunapata mshahara mmoja kwa kuwa tunafanya kazi ya mtu mmoja kwa pamoja lakini katika siku zijazo tunafikiria kuongea na mabosi zetu watuongezee mshahara au kila mtu apewe mshahara wake maana tuna Degree mbili kila mtu yake.

"Pia tunao uwezo wa kufundisha masomo tofauti kila mmoja au kufundisha kwa njia tofauti, mfano mmoja anaweza kuwa anafundisha huku mmoja anasimamia uelewa wa Wanafunzi na kujibu maswali Yao,"  alisema Abby.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live