Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Manusura wa ajali ya ndege walivyokua maiti za wenzao ili waishi

Ajaliii371567 Manusura wa ajali ya ndege walivyokua maiti za wenzao ili waishi

Sat, 20 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya raga ya shule ya Old Christians Club kutoka Montevideo, Uruguay ilikodi ndege ya Jeshi la anga la Uruguay kusafiri Oktoba 13, 1972 hadi Santiago, Chile.

Wakisafiri kwenda kucheza mechi dhidi ya Old Boys katika jiji hilo. Ndege yao FH-227D, iliyokuwa na abiria 45, ilipokuwa ikivuka Milima ya Andes, ilianguka na kusababisha vifo vya papo hapo vya watu 12.

Wengine 17 walikufa siku zilizofuata, kutokana na majeraha, ukosefu wa chakula na hali mbaya waliyokabiliana nayo.

Ajali hiyo ilipachika jina la "Muujiza wa Andes" na imeonyeshwa katika filamu ya Netflix "The Snow Society."

Ni moja tukio la kushangaza katika historia ya anga kwani watu16 walionusurika ni kwa sababu walikula miili ya wenzao waliokufa. Waliokolewa siku 72 baada ya ajali hiyo.



Mmoja wa waliookolewa, Roberto Canessa, sasa ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto. Alihojiwa na BBC, Machi 2016, baada ya kutoa kitabu chake cha ushuhuda wa tukio hilo.

Tukiwa katika anga ya Andes kulikuwa na mawingu sana. Wakati fulani mmoja wa wahudumu wa ndege aliwaambia abiria "fungeni mikanda, tutapitia katika mawingu na ndege itatetemeka."

Hakika, ndege ilianza kutetemeka. Kuna mtu aliniambia nichungulie dirishani, ndege ilikuwa ikipaa karibu sana milima.

Ndege ilijaribu kupaa kwenda juu urefu, lakini ilianguka. Nilishikilia kiti changu bara’bara. Ndege ilipoteza mabawa yote mawili na kuanza kuteleza chini ya milima.

Hatimaye iliposimama, niliruka kwa nguvu na niligonga kichwa changu na ardhi kwa nguvu na kuhisi kama nitazimia. Sikuamini kwamba ndege ilikuwa imesimama.

Niliona miguu yangu bado ipo, mikono yangu bado ipo, nimeokoka.

Chanzo cha picha, URUGUAYAN AIR FORCE

Maelezo ya picha, Picha ya mabaki ya ndege.

Sikuweza kuamini. Niliangalia pande zote na kila kitu kimetawanyika. Baadhi ya marafiki walikuwa wamekufa, wengine walijeruhiwa, wakivuja damu, wengine walikuwa na vipande vya vyuma miilini mwao.

Nilijisemea ni lazima niodoke hapa, polisi watakuja, magari ya kubebea wagonjwa yatakuja, askari wa zima moto, nikaenda kwenye mkia wa ndege.

Ndege ilivunjika na nilipokwenda kwenye theluji, nilihuzunika sana kwa sababu tulikuwa katikati ya milima, tukiwa tumezingirwa na ukimya mkubwa.

Hakukuwa na msaada wowote

Rubani alikuwa hai, lakini alinasa kwenye chumba cha marubani. Hawakuweza kumtoa na akasema "Kuna bunduki kwenye mkoba wangu." Alitaka kujiua. Aliugulia uchungu usiku kucha. Hatukuweza kumtoa.

Baridi ilikuwa kali. Siku iliyofuata, aliyejeruhiwa vibaya walifariki. Nilijisikia vyema kwa sababu alikuwa akipata mateso na maumivu makali.

Kwa wale waliobaki, kulikuwa na miamba na theluji tu. Hakukuwa na chakula na tulihisi njaa. Kuna hisia ndani yako inakwambia unapaswa kula kitu. Kwa hiyo tulifikiria kula ngozi ya viatu au kamba.

Tulianza kutafuna ngozi, lakini tulihisi ilikuwa na sumu, kwa sababu ilikuwa na kemikali nyingi. Kwa hiyo hatukuweza kuendelea kutafuna.

Kula Binadamu

Mtu mmoja wakati fulani alisema, "Nadhani nimepata wazimu, kwa sababu nafikiria kula miili ya marafiki zetu."

Walijibu huo ni wazimu, hatutafanya hivyo, hatutakula nyama za watu.

Wakati huo, nilikuwa mwanafunzi wa udaktari na niliona nyama, mafuta, protini, wanga. Ilikuwa vigumu kwangu kukata sehemu ya miili yao.

Mtu mwingine alisema , "ikiwa Yesu Kristo alisema kwenye Karamu ya Mwisho uchukue mwili wangu na damu yangu."

Lakini kwangu haikuwa Karamu ya Mwisho. Ingawa wakati huo nilijiuliza ninge "waza" nini ikiwa ningekuwa mmoja wa maiti.

Ningejivunia kwamba mwili wangu ulitumiwa na marafiki zangu kwa riziki. Leo nahisi nina sehemu ya marafiki zangu ndani yangu na sina budi kushukuru kwa kumbukumbu zao.

Kula miili ili kuishi muda mrefu zaidi ili kuokolewa, ilikuwa vigumu kwa wengine lakini rahisi kwa wengine.

Mara ya kwanza ilikwua kama majaribio. Kisha ikawa kawaida kukata nyama na kugawana kati ya waliosalia.

Mshikamano

Familia (za marehemu) zilituunga mkono, hawakujali kilichotokea kwa miili hiyo, walijali kilichotokea wakiwa hai.

Inafurahisha kwa sababu katika tukio hilo nadhani kuna mambo mawili. Jinsi tulivyoishi na tulivyokula maiti.

Watu husema "ah, ulinusurika kwa sababu ulikula maiti," kana kwamba ni jambo la makusudi.

Kula miili ilikuwa ni kununua tu wakati. Tulinusurika kwa sababu tulikuwa timu, tulifanya kazi pamoja, tulisaidiana.

Tulinusurika kwa sababu tuliondoka milimani na kutembea kwa siku 11. Moja ya jambo ambalo lilitusaidia - tulikuwa kikundi, tulikua pamoja.

Nilipokuwa milimani na kuona marafiki zangu wamekufa, nilijua nami ningeweza kufa na nilitambua jinsi mstari wa maisha na kifo ulivyokuwa mwembamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live