Kupitia mitandao ya kijamii tangu jana asubuhi zinasambaa picha za mwanamitandao na Blogger maarufu nchini anayeishi Marekani Mange Kimambi zikionyesha ameolewa rasmi.
Picha hizo zinaonyesha Mange akiolewa na Mzungu wake ambaye mara nyingi amekuwa akimzungumzia mitandaoni.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Mange hajapost chochote lakini marafiki zake Hamisa Mobetto na Mwamvita makamba wamethibitisha hilo kwa kumpongeza na kuingia kwenye ndoa yake.
Aidha, Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amempongeza Mange kwa hatua hiyoo;
Hatimae Mange kaolewa tena bhana, usikate tamaa hadi Ufe dadadeki. Kweli au? Kama Kweli ikawe kheri harusi yake na tunategemea sasa ataachana na ndoa na mahusiano ya Watu, aendelee kuupiga mwingi na Mzungu wake!!
"Naambiwa huyo Mdhungu ni Mzibua Vyoo maarufu huko US, Kiufupi choo kikimuona tu kabla ya kukigusa kinazibuka chenyewe. All in All safi hii, utulie sasa na uache midanga, Bata Wahed," ameandika Manara.