Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maneno yamkimbiza Uwoya kwa Kayumba

3b1e7178e99330e4261ae43e25f4fd75 Maneno yamkimbiza Uwoya kwa Kayumba

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSHINDI wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS) mwaka 2015, Kayumba Juma, amesema ilibaki kidogo mwigizaji nyota Irene Uwoya awe meneja wake, lakini maneno ya watu yalimkimbiza.

Akizungumza na Wasafi Tv, msanii huyo alisema Uwoya alionesha nia ya kumsimamia muziki wake ila kutokana na namna walivyokuwa yakaibuka maneno kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanatoka pamoja.

“Uwoya alitaka kunisimamia katika muziki wangu kwa hiyo tukaanza kupiga picha na kuweka kwenye mitandao ndipo maneno yakaibuka kuwa tunatoka pamoja na yeye hakuyapenda kwa sababu ni mtu mwenye familia yake hivyo akaamua kuachana na mimi,” alisema.

Alisema kwa sasa anapambana mwenyewe na meneja wake ingawa bado hajapata uwekezaji wa kutosha kufikisha mbali muziki wake.

Kayumba alisema amekuwa akipiga hatua taratibu ila anatamani angekuwa kwenye lebo kubwa kama Wasafi au Kings music record ili aweze kufika mbali zaidi.

Alisema anajipa moyo akiamini ipo siku mambo yatakuwa mazuri kwani anaweza kuimba wimbo wa pamoja na mkongwe wa muziki huo Ali Kiba kwa kuwa yupo naye karibu na amekuwa akimuunga mkono.

Chanzo: habarileo.co.tz