Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandojo na Domokaya, The Bongo Flava Perfectionists!

Mandojo Domokayaaa(19).jpeg Mandojo na Domokaya.

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ulikuwa wapi Bongo Flava ilipoitwa muziki bazoka? Utamu wake ni ule upya. Mithili ya bubble gum, ladha inaisha haraka mdomoni, inatemwa.

Kejeli, dhihaka, viliisindikiza Bongo Flava kadiri ilivyochanua. Bongo Flavas wakaitwa wabana pua, sio wanamuziki. Utabiri ukatolewa, ngoma ya watoto haikeshi, Bongo Flava ingetoweka ndani ya muongo mmoja.

Majanki wawili, wao kubeba guitar ni kama daktari na stethoscope. Walijikabidhi dhima ya kuivalisha Bongo Flava joho la heshima. Wape guitar wajisikie wapo nyumbani. Wakulipe fadhila kwa burudani kali live.

Wanasayansi Mandojo na Domokaya, waliondosha dhana kuwa Bongo Flavas ni wasanii wa studio tu. Yeyote angekebehi Bongo Flavas ni studio artists only, angejibiwa; je, Mandojo na Domokaya?

Genius scientists; Dojo na Domo, hawakuandika nyimbo, walitunga muziki. Kila wimbo, from singing melodies to the guitar, chords zilisoma perfectly. Ilimchukua saa chache P Funk kukamilisha “Nikupe Nini”.

Dojo na Domo walipotua FM Studio kwa Mika Mwamba, kila wimbo ulikuwa clean kuanzia melodies, harmony, key, metre na rhythm. Albamu “Taswira” ilikamilika kufumba na kufumbua.

Kisha “Mika anasema usimwache aende... mwache aende... kaniacha niende.” Ngoma inaitwa “Nizikwe Hai” iliyobeba jina la albamu. Halafu kuna “Dingi”. Ni baraza la kifamilia kati ya baba msela mavi aliyekimbia majukumu na mtoto mwenye machungu ya kutelekezwa.

Dojo na Domo ni mini-sized orchestra. Wapo huwatafsiri kama Hip Hop Banjo superheroes. Ukiogopa dhambi utawaita the Bongo Flava perfectionists.

Ingizo lao sokoni limei-perfect Bongo Flava kuanzia kuutoa muziki studio na kuupeleka live, vilevile style yao ni unmatched. Sanaa ya Dojo na Domo ime-cement sound ya Bongo Flava.

Kutotambua athari ya Dojo na Domo kwenye Bongo Flava ni kujipeleka jehanamu kizembe. Bongo Flava Honors Academy, imejitenga na dhambi inayoepukika.

Septemba 29, 2023, haitakuwa induction ceremony ya Dojo na Domo, isipokuwa udhihirisho kuwa wao ndio miniature orchestra wa Bongo Flava. Dakika 120 live jukwaani with Swahili Blues Band. See you in the venue; Alliance Francaise, Upanga.

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live